Polisi mkoani Tanga, inawashikilia watu wanane kwa tuhuma za uhalifu ambao inadaiwa walitoka jela kwa msamaha baada ya kufanya matukio mbalimbali ya ujambazi wa kutumia silaha.
Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Mkoa wa Tanga, Henry Mwaibambe amesema watu hao ni wahalifu wa makosa mbalimbali ya uporaji wakutumia silaha.
Amesema, “tunawashikilia watu nane ambao wana makosa mbalimbali ikiwamo uporaji wa kutumia silaha na wengine wanatafutwa katika mikoa ya jirani, wapo ambao walimaliza vifungo gerezani.“
Kutokana na tukio hilo, Kamanda Mwaibambe amewaomba Wananchi kusherehekea sikukuu kwa amani na pia wajiepushe na vitendo vya kihalifu ikiwemo uvunjifu wa sheria za barabarani.