Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa onyo kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanaofanya kazi za kisiasa badala ya kitendaji ili hali kwenye maeneo yao zimepelekwa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Waziri Mchengerwa amesema hayo Oktoba 17, 2023 kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Samora, Nzega  mkoani Tabora wakati akimkaribisha Rais  Dkt.Samia Suluhu Hassan kuzungumza na Wananchi waliojitokeza kumsikiliza.

“Mhe. Rais tunatambua kiwango cha Fedha unachopeleka kwenye Mikoa na  Halmashauri ni kikubwa sana, lakini tunao baadhi ya Wakuu wa Wilaya na baadhi ya Wakuu wa Mikoa ambao maeneo yao yamepokea fedha nyingi za Miradi ya maendeleo na kwa bahati mbaya baadhi yao wengi wao wamekuwa wakifanya kazi za Siasa kutafuta Majimbo kwenye baadhi ya maeneo badala ya kufanya kazi ya kusimamia miradi ya maendeleo.”

“Mhe. Rais wakati unatuapisha tulikuahidi tutakuletea orodha ya baadhi ya Wakuu wa Wilaya ambao hawafanyi kazi ya kusimamia miradi ya maendeleo ambapo unapeleka Fedha nyingi  sasa ni wakati wa kuleta orodha hiyo ili wakajipange vizuri kwenye Siasa na pale upeleke Watu ambao wataweza kufanya kazi ya kusimamia miradi ya maendeleo,”amesema.

Amesema fedha zinazopelekwa kwenye Halmashauri na  Mikoa ni nyingi  zinahitaji usimamizi wa karibu.

Ally Mayay amkumbusha Karia na TFF yake
Carlo Ancelotti akataa kazi Brazil