Shirika la Afya Duniani (WHO) limeorodhesha kuwa michezo ya video yani ‘video games’ kama mchezo ambao unachangia ugonjwa wa akili.
Katika ripoti iliyotolewa na WHO imesema kuwa hali hii inaathiri asili mia tatu ya wachezaji wa michezo hiyo huku muda mwingi wakipoteza kwa kukaa na kucheza mchezo huo ambapo kwasasa unashika kasi kubwa.
WHO imesema kuwa kuna baadhi ya watu hucheza ‘video games’ bila hata kufikiria, jambo ambalo linawafanya wategemee sana michezo hiyo, huku wengine huachana na shughuli zao za kawaida ili kucheza michezo hiyo, kwani wasipofanya hivyo, huonekana wanyonge na wadhaifu.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press, limesema kuwa zaidi ya watu bilioni mbili duniani wanacheza michezo ya aina hiyo.
Aidha, tayari kuna kituo cha matibabu kilichofunguliwa Los Angeles na California nchini Marekani ambacho kinawahudumia watu kisaikolojia ili kuweza kuachana na michezo wa video games.
-
Merkel, Macron wateta kuhusu mzozo wa Umoja wa Ulaya
-
Mali za mpinzani wa Kagame zapigwa mnada nchini Rwanda
-
Trump aitishia China, watunishiana misuli
Hata hivyo, WHO imeonya kuwa iwapo vijana hawatapunguza mazoea ya kucheza ‘video games’ basi hali hiyo itakuwa mbaya siku za mbeleni kwa ongezeko la watu wenye ugonjwa.