Watu wane kati ya sita wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuwawa baada ya kutokea kwa mapigano ya kurushiana risasi na Jeshi la polisi mkoani Lindi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi Kamishina Msaidizi Mtatiro Kitinkwi amesema kuwa walipata taarifa za kintelijensia za kuwepo kwa kundi la majambazi linaloelekea kufanya tukio katikati ya Wilaya ya Ruangwa na Nachingwea barabara ya Nanganga.
Amesema, kwa kutumia doria ya pikipiki, waliweka mtego katika maeneo hayo.
Kamanda Mtatiro amesema baada ya muda zilitokea pikipiki mbili zilizokuwa zimepakia mishikaki kila moja ilikuwa na abiria wawili , wawili, waliposimamishwa Kwa lengo la kuhojiwa walikaidi na ndipo walianza kurushiana risasi na Polisi.
Aidha amesema kuwa katika majibizano hayo ya risasi, watu wanne walijeruiwa na kukimbizwa hospital ya mkoa ya Sokoine wakiwa njiani walipoteza maisha.
Kamanda Mtatiro ametoa onyo kali kwa wahalifu wanaojaribu kuja kufanya uharifu katika mkoa Lindi.