Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt Mwigulu Nchemba ameagiza kutafutwa na kukamatwa mara moja kwa watu wote wanaohusika na uteswaji wa vijana wanaopelekwa nje ya nchi kutafuta ajira.
Ameyasema hayo hii leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kupata taarifa ya mateso wanayopata baadhi ya wananchi wa Tanzania wanaokwenda kufanya kazi tofauti tofauti nje ya nchi.
Amesema kuwa wameshafanya mawasiliano na Wizara zote zinazohusika na wameshakubaliana kila mmoja kuchukua hatua kulingana na wizara yake.
“Wale watu wanaoweka rehani vijana wetu, wamekuwa wakikimbia hapa na pale na ambao bado hawajakamatwa mpaka sasa waendelee kusakwa wote na wafikishwe katika mkono wa sheria ili sheria iweze kufuata mkondo wake kwa vitendo hivyo vya kinyama,”amesema Dkt. Nchemba
-
Mrisho Mpoto atoa msaada kwa yatima, ‘nimeamua kugawana na watoto kidogo nilichojaliwa
-
RC Masenza awaonya watumishi wa Serikali
-
Amuua mpenzi wake kisha aandika ujumbe mzito
Hata hivyo, Nchemba ameongeza kuwa matatizo wanayoyapata vijana hao kwa kisingizio cha kupatiwa kazi nje ya nchi mpaka sasa yamekuwa makubwa na hayavumiliki.