Wanariadha 21 wamepoteza maisha yao kutokana na hali mbaya ya  hewa katika mbio za kilometa 100, ambazo pia zilijumuisha kupanda mlima.

Katika marathon iliyoanza katika jimbo la Gansu Jumamosi asubuhi, wanariadha 172 walianza kukimbia kama ishara ya kuanza.

Wakati wa mbio hizo za kilometa 100, hali ya hewa ilizorota ghafla, ikawa baridi na mvua ikaanza kunyesha, na kupelekea wanariadha kukwama katika eneo hilo.

Baada ya hali hiyo kutokea , operesheni ya kuokoa wanariadha ilianza.

Wanariadha 151 kati ya 172 wameokolewa, wakati 21 wamepoteza maisha.

Kiongozi Young Africans aikubali Simba SC
Wabunge wapya waapishwa