Satelaiti ya zamani ya NASA inatarajiwa kuanguka duniani wiki hii, huku Wataalam wanaofuatilia chombo hicho wakisema uwezekano wa uharibifu ni mdogo na kwamba haitaleta hatari yoyote.
Kwa mujibu wa taarifa ya idara ya ulinzi ya NASA, imesema Satelaiti hiyo iliyokufa inayojulikana kama Reuven Ramaty High Energy Solar Spectroscopic – Rhessi, yenye uzito wa kilo karibu 300 inatarajia kuporomoka angani hii leo April 20, 2023 na bado haijulikani ni eneo gani itaangukia.
Sehemu kubwa ya satelaiti hiyo yenye thamani ya pauni 660 ilitengenezwa na kikundi cha wanaanga kwa safari za anga huku ikisisitiza kuwa hakuna hatari ya mtu yeyote Duniani kudhurika na kwamba awali ilirushwa kwenye obiti mwaka 2002 ili kusoma mwenendo wa jua.
Hata hivyo Satellite hiyo ilizimwa mwaka 2018 kwa sababu ya matatizo ya mawasiliano, baada ya kuona miale ya ukinzani wa miiko ya jua iliponasa picha katika X-ray yenye nishati nyingi na miale ya gamma, ambapo ilirekodi zaidi ya matukio 100,000 ya jua.