Wanasayansi wameibuka tena na kudai chini kabisa ya Bahari ya Hindi, kuna “shimo la mvuto” ambalo lina ukubwa wa zaidi ya maili za mraba milioni moja ambao umewashangaza.
Ingawa kitaalam si shimo la kawaida, Mwandishi Victor Tangermann wa jarida la the byte, anasema wanajiofizikia hao wametumia neno “Indian Ocean geoid low – IOGL”, kuashiria eneo lilipo ambapo athari za mvuto wa Dunia ni wa chini kuliko wastani.
Hata hivyo, wanasayansi hao wanasema huenda wamegundua jinsi hali hii isiyoeleweka yenye muonekano wa kuvutia kuwa ni mageuzi ya kijiolojia ya sayari hii ya kale.
Aidha, wanasema hakuna athari zozote ingawa shimo hilo la Indian Ocean geoid low – IOGL, na muonekano wake katika ramani ni kama umbo la kiazi na linazidisha milima na mabonde yenye uvutano.
Hata hivyo, wanasema wamebaki na maswali mengi ambayo bado hayana majibu na kwamba tafiti zaidi zitaendelea ili kupata uhalisia wa shimo hilo na kisha kuendeleza hatua inayofuata.