“Naomba nijitambulishe ili ninapozumgumza mtapata fursa ya kujua kama nazungumza kitu nachokijua au na mimi nabahatisha kama wale wengine ambao wamebobea kwenye mambo ya mirathi na masuala ya mazingira. Wanaopinga Mkataba wakitaka kutuaminisha kuwa wao hawawezi kukosea.”

Ni nukuu ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni na  Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Wakili wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Albert Msando wakati akiongea katika Mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi – CCM jijini Mwanza hii leo Julai 30, 2023.

Msando amesema, “jana nimesikia ndugu yangu mmoja akiwa Kagera huko, anasema kuna watu wamefundishwa na maprofesa. Kwa hiyo wanataka kutuaminisha kuwa wao hawawezi kukosea. Sasa mimi nimjibu, Profesa anayemzungumzia na mimi amenifundisha na ndiye alinisimamia kwenye utafiti wa degree yangu ya kwanza ya Sheria.”

Mwanasheria huyu anaongeza kuwa, “lakini pia vile vile nina degree ya pili ya ubobezi kwenye sheria na nina degree nyingine ya ubobezi kwenye utawala wa umma. Na nimefanya kazi ya uwakili kama wakili wa kujitegemea kwa zaidi ya miaka 17. Kwa hiyo nimeandaa mikataba, nimesoma mitakaba na nina ielewa.”

Tanga yatarajia kuzalisha Wanasayansi Mahiri Kitaifa
Lushoto hawajakata tamaa, wana jambo lao