Watu watatu waliokodi chumba cha kulala katika nyumba ya kulala wageni mtaani Pipeline katika Kaunti ya Nairobi nchiuni Kenya wamepatikana wakiwa wamefariki ndani ya chumba hicho.
Watatu hao, wanaume wawili na mwanamke mmoja, walikodi chumba hicho mwendo wa saa sita na dakika 35 usiku wa kumkia Jumatatu, Mei 9 katika nyumba ya wageni ya Chairman mtaani Pipeline na kubakia chumbani humo hadi saa nane mchana.
Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, mhudumu wa vyumba hivyo alienda kufuatilia baada ya watatu hao kutoondoka na kukuta mlango ukiwa umefungwa kwa ndani.
“Alienda kuwaamsha lakini baada ya kugonga kwa mlango wao hukukuwa na jibu lolote jambao ambalo lilimfanya kuarifu bosi wake na moja kwa moja kupiga ripoti kwa polisi,” taarifa ya polisi inasema.
Polisi walipofika waliingia chumbani kwa nguvu kwa kuvunja vioo vya mlango na kuikuta miili ya wanaume wawili na mwanammke mmoja ikiwa imelala kitandani.
Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, watatu hao walikuwa wameshikana mabegani na kila mmoja alikuwa amefunga mdomo wake kwa nguvu. “Hakukuwa na majeraha yoyote yanaoonekana au ishara ya vurugu. Lakini mwanamme ambaye alikodi chumba hicho kwa jina Boniface Muchiri Waruiru alikuwa ametokwa damu mdomoni na puani,”
Taarifa hiyo iliongeza. Vitambulisho viwili vya kitaifa vilipatikana chumbani humo vikiwa na majina Philip Murefu Simiyu (kuzaliwa 1959) and Boniface Muchiri Waruiru (kuzaliwa 1994). Miili ya watatu hao ilipelekwa katika Hifadhi ya Maiti ya City inakosubiri kufanyiwa upasuaji kubaini chanzo cha vifo hivyo.