Wataalamu wa afya sasa wameonya kuwa wanaume wanaovalia nguo za ndani zilizobana sana na kuoga maji moto kwa muda mrefu wanajiweka katika hatari ya kuwa tasa.

Kulingana na wataalamu hao, nguo za ndani zilizobana sana na maji moto husababisha joto jingi kupita kiasi katika korodani ambapo mbegu za kiume hutengenezewa kwa kuwa Mbegu za kiume hutengenezwa katika mazingira ya joto la sentigredi 34 ambalo ni chini ya joto la kawaida la mwili la sentigredi 36.

Mbegu huwa dhaifu zinapotengenezewa katika mazingira yenye joto jingi zaidi ya sentigredi 34. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Harvard nchini Marekani, ukiwashirikisha wanaume 656, ulibaini kuwa asilimia 75 ya waliovalia nguo za ndani na suruali za kubana walikuwa na mbegu hafifu.

Hali hiyo ilikuwa tofauti na wanaume waliokuwa wamevalia nguo ambazo hazijabana mbegu zao za kiume zilikuwa bora na nyingi.

Utafiti mwingine uliofanywa na Chuo Kikuu cha Stanford, Marekani, nao ulionyesha kuwa kuvaa nguo zilizobana usiku kunasababisha mbegu za kiume kuharibika.

Katika utafiti mwingine sawa na huo uliofanywa na Chuo Kikuu cha California, ulifichua kuwa kukalia au kuogelea kwenye maji moto kwa muda mrefu kunasababisha mbegu za kiume kuwa hafifu.

Hatua ya kufanya Kutokana na athari hizo, wataalamu wanashauri wanaume kuoga au kuogelea kwenye maji moto kwa muda usiozidi dakika 30 kwa wiki.

Hata hivyo, kando na kuoga maji moto na kuvaa nguo zilizobana, wataalam hao wanahoji kuwa mambo mengine yanayofifisha mbegu za kiume ni msongo wa mawazo, matumizi ya baadhi ya dawa, dawa za kulevya na kupumua hewa chafu iliyo na kemikali kama vile dawa ya kunyunyizia mimea.

Vile vile mihadarati kama vile bangi na kokeni inaua mbegu za kiume vilevile zinaonyesha kuwa bangi inasababisha mbegu za kiume kuwa mbovu na kubadili umbo.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Machi 10, 2022
Akataa kurudisha Mamilioni ya Dola alizofidiwa kimakosa