Taarifa za kiutafiti zinaonesha kuwa Mwanaume ni mgumu wa kufanya kile anachotakiwa au kuombwa kukitekeleza na mkewe kwani nyuma ya ubongo wake, kuna kizuizi ambacho kinachopingana na chochote kile ambacho Mwanamke anamtaka kukifanya.
Utafiti huo wa hivi karibuni ambao uliongozwa na Profesa wa Masoko na Saikolojia, Gavan Fitzsimons wa Chuo Kikuu cha Duke kilichopo Durham North Jimbo la Carolina nchini Marekani unaeleza kuwa, kinachotokea ni Mwanaume kutotaka kupangiwa kwenye mambo yake, bila mwenyewe kujua kwamba anafanya juhudi hiyo.
Aidha, jambo hilo kisaikolojia linafahamika kama “reactance”, ambapo mtu hufanya kinyume kabisa na anavyotakiwa kufanya yaani juhudi za mtu kupinga kupewa amri au kuingiliwa katika uhuru wake kimaamuzi.
Hata hivyo, Wataalamu wanasema Wanaume hujikuta wamepinga jambo la mke bila kujua hata sababu na ndio maana wengi wao huharibikiwa kwa kukataa kufanya yaliyopendekezwa na wake zao na baadae hujiuliza ni kwa nini walikataa ama kujutia.
Ushauri: Mwanaume unapaswa kujua kwamba, unapoombwa jambo na mwenza wako au kutakiwa kufanya kitu fulani, kwanza utakuwa katika hatari ya kulikataa, hivyo ukijishtukia upo katika hiyo hali shtuka na kuwa mwangalifu, chekecha na fanyia kazi.