Serikali wilayani Nkasi mkoa wa Rukwa imewaonya wanaume na kuwataka waache mara moja tabia ya kuwaita wanafunzi wa kike majina ya kimapenzi kwa kuwa yanasababisha wajione watu wazima hivyo kushawishika kufanya ngono.
Onyo hilo limetolewa na Ofisa Elimu (Sekondari) Wilaya Naksi, Abel Ntupwa katika kikao cha kazi kilichowashirikisha wakuu wa shule za Sekondari 23.
”Tabia hiyo ni mbaya na haikubaliki ni marufuku kwa mwanaume yeyote kumuita mwanafunzi wa kike majina ya mahaba kama ‘baby’, ‘my love’, ‘my sweet’ ili kuwaepusha na ujanja wa wanaume na kuwalinda dhidi ya mimba za utotoni ili watimize ndoto zao, amesema Ntupwa.
-
NASA wabadili gia, wapanga kumuweka Raila kwenye kiti cha Kenyatta
-
UVCCM yakamata gari la Meya wa Jiji
Amekemea tabia hiyo ya baadhi ya wanaume kujihusisha kimapenzi na wanafunzi hao.
Aidha amewaonya walimu ambao wanatabia ya kuwatamani wanafunzi na kusema kufanya hivyo ni dhambi kubwa sana, na kuahidi kuwachukulia hatua kali walimu wanaofanya na kuendelea na tabia hiyo.
Pia amewasisitiza walimu wakuu kusimamia ipasavyo na kuhakikisha walimu wanafanya kazi moja tu ambayo ni kiuwafundisha watoto na sio kuwatamani.
.