Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametia saini agizo la kuwataka wananchi wake wajiandae kwa ajili ya ulinzi wa nchi yao ambapo amewataka wanaume wenye umri kati ya miaka 18 hadi 60 kutokimbia ili waendelee kulinda nchi yao kutokana na uvamizi wa Urusi.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken anasema “anashawishika” kwamba rais wa Urusi Vladimir Putin atajaribu kupindua serikali ya Ukraine.

Blinken alisema ni sehemu ya mpango wa Urusi kushambulia mji mkuu wa Kyiv na miji mingine mikubwa nchini Ukraine, pamoja na kuanzisha mashambulizi ya pande nyingi dhidi ya nchi hiyo kutoka kaskazini, mashariki na kusini.

Alisema shambulio la Urusi nje ya Ukraine lingwezekana lakini akasisitiza kujitolea kwa Marekani katika kuwalinda washirika wake wa Nato, akionya kuwa shambulio dhidi ya mwanachama mmoja wa Nato ni shambulio kwa wanachama wote wa Nato.

“Rais amekuwa wazi kwamba tutalinda kila inchi ya eneo la Nato. Nadhani hicho ndicho kizuizi chenye nguvu zaidi dhidi ya Rais Putin kwenda nje ya Ukraine” alisema.

Alisisitiza msimamo wa Rais wa Marekani Joe Biden kwamba uwezekano wa kupanua vikwazo vilivyopo vya Marekani kumlenga Putin moja kwa moja bado uko mpangoni ikiwa hali itazidi kuwa mbaya.

Dodoma yaja na mbinu za kutakatisha Jiji
Uzalishaji wa madini Joto kuongezeka Tanzania