Takwimu za Shirika la Idadi ya watu ulimwenguni UNFPA zinasema Wanawake 8,000 hadi 11,000 hufariki kila mwaka kwa sababu zinazotokana na ujauzito.

UNFPA imeongeza kuwa sababu hizo zinaweza kuzuilika kwa kuongeza jitihada za pamoja kuwapa kipaumbele wakunga ambao wamekuwa msaada katika maswala ya uzazi kuanzia ngazi ya jamii mpaka Taifa.

Akiongea na vyombo vya Habari, Katika maadhimisho ya Siku ya wakunga duniani, Msimamizi wa Mradi wa Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto – UNFPA , Felista Bwana amesema wanawake wengi hufariki kutokana na kutokwa damu nyingi wakati wa kujifungua na kifafa cha uzazi kwa karibu asilimia 50.

Amesema, “sababu hizi nyingi zinazuilika na asilimia kubwa ya wanawake hufa kwa kukosa msaada wa haraka, endapo wakunga hawa wangepatiwa vifaa maalum na kupewa elimu zaidi basi kila kituo cha afya kuanzia ngazi ya jamii ingepunguza vifo hivi na hatimae kufikia lengo la asilimia sifuri kwa mwaka 2030.”

Aidha, kwa upande wake Mkuu wa Miradi kutoka Wizara ya Afya Dk Catherine Joachim amesema pamoja na juhudi ambazo zinafanywa na wadau bado tatizo hilo ni kubwa na juhudi za ziada zinahitajika katika mapambano hayo na serikali inaendelea kuboresha hali ya wakunga Nchini Tanzania.

Naye Mwakilishi Mkaazi wa UNFPA nchini Mark Bryan Schreiner, amesema 15% ya wajawazito nchini hawajifungulii kwenye huduma stahiki za afya kwa kukosa wataalamu ambao ni wakunga.

Amesema Katika nchi nyingi duniani Wakunga ndio watu wa muhimu katika jamii ambao hueneza elimu tofauti za kijamii kuanzia elimu ya Kujamiiana na afya ya uzazi na kusaidia wajawazito kujifungua salama katika maeneo ambayo hayafikiki kwa urahisi.

Nae makamu wa rais wa chama cha wakunga Tanzania TAMA ameweka msisitizo kuwa “Sio kila mtu anaezalisha anaweza kuitwa mkunga, na hapo ndipo jamii inapotoshwa kwa kuamini wakunga ni wengi, Mkunga ni yule mtaalamu ambaye amepotia elimu ya ukunga kutipitia chuo cha ukunga na kupata maarifa ya kitaalamu juu ya masuala yote yanayohusu ukunga. Huyu ndie mkunga”

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Mei 6, 2023
TMA yafuatilia mifumo hali ya hewa uwepo mvua za El Nino