Mbunge mmoja nchini Urusi amewataka wanawake kutofanya mapenzi na raia wa kigeni wakati wa kombe la dunia huku akionya kuhusu watoto wanaozaliwa kutoka rangi tofauti.
Tamara Plentyova mkuu wa kamati ya familia, wanawake na masuala ya watoto bungeni, amesema kuwa hata kama uhusiano huo utasababisha kufanyika kwa harusi, wanawake au watoto wao watachukuliwa na wanaume hao ambao watakuwa raia wa kigeni.
”Hata wakiolewa, watawachukua, halafu watashindwa namna ya kurudi,”amesema Pletnyova katika kituo cha Govorit Moskva.
Aidha, amesema kuwa wanawake waliopata watoto na raia wa kigeni wakati wa michezo ya Olimpiki ya mwaka 1980 mjini Moscow walibaki kuwa wanawake wasio na wanaume huku watoto wenye asili ya rangi nyeusi wakiitwa watoto wa Olimpiki.
Hata hivyo, zaidi ya watalii milioni moja wa kigeni wanatarajiwa kuhudhuria kombe la dunia, suala linalozua wasiwasi kuhusu ubaguzi wa rangi.
-
Trump, Kim Jong Un wasaini makubaliano
-
IMF yaonya kuhusu sera za Marekani
-
Salva Kiir, Machar uso kwa uso Ethiopia