Chama cha waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar – TAMWA-ZNZ, kimewataka Wanawake kuwa na ujasiri na kujitayarisha kiuongozi bila kuogopa changamoto zinazowakabili pale wanapoingia katika uongozi, ili kuongeza ushiriki wao kwenye vyombo vya maamuzi.

Hatua hiyo, imekuja kufuatia uwepo wa idadi ndogo ya wanawake katika vyombo vya maamuzi na michakato ya kidemokrasia ambao umejidhihirisha katika chaguzi zinazofanyika nchini na wanawake kupata nafasi chache kitu ambacho ni kikwazo cha kuimarisha demokrasia.

Aidha, katika kupambana na hali hiyo TAMWA ZNZ pia imeendesha mafunzo kwa wanawake wenye dhamira ya kugombea nafasi za uongozi Zanzibar na kubaini kwepo kwa hofu miongoni mwa wanawake kushiriki katika nafasi hizo kutokana na sababu mbalimbali.

Miongoni mwa sababu zilizobainika kukwamisha ushiriki wa wanawake katika vyombo hivyo ni vitisho, hofu dhidi ya rushwa ya Ngono, pamoja kukosekana kwa mifumo na sera ya jinsia ndani ya vyama vya siasa inayowajenga na kuwaandaa wanawake kuwa viongozi bora.

Sababu nyingine ni kukosekana kwa mifumo hiyo kunaathiri uwezo wa wanawake kutambua na kusimama kudai haki zao za msingi jambo ambalo ni kinyume na matakwa ya katiba na mikataba ya kimataifa kuhusu haki za kibinaadamu.

Changamoto hiyo, imepelekea wanawake wengi kujaribu kuingia bila kuwa na misingi sahihi ya namna ya kuwa kiongozi bora na kuweka ugumu wa ufikiaji wa lengo namba tano la Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa linalohimiza upatikanaji wa Usawa wa Kijinsia kwa Wanawake na Wasichana katika nyanja zote.

Pape Osmane Sakho aondoka Simba SC
Taaluma ya Uuguzi ni kazi ya uthubutu - Kikwete