Serikali imesema kuwa inapeleka hoja ya kuondoa riba ya asilimia 10 kwenye mikopo ya wanawake na vijana inayotolewa na halmashauri zote hapa nchini.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Selemani Jafo wakati wa uzinduzi wa mpango wa kukuza utalii jijini Dar es salaam.
Amesema kuwa utekelezaji wa agizo hilo utaanza mwaka ujao wa fedha baada ya kuliingiza jambo hilo kwenye bajeti kuu ya serikali itakayowasilishwa bungeni.
“Sitaki kusikia mikopo hiyo inatolewa kwa riba, hizo ni fedha za wananchi na wengi wanaokopa ni wale wenye shida sana, jambo hili la riba sitaki kulisikia,”amesema Jafo
Hata hivyo, halmashauri nyingi tayari zimesha kopesha vikundi vya vijana na wanawake fedha kwa rejesho la asi;limia 10 ya riba ya mkopo wote.