Nchi ya Taliban imesema Wanawake wanaotaka kusafiri umbali mrefu (zaidi ya Kilomita 72) wasipewe usafiri barabarani isipokuwa wakiwa wamesindikizwa na ndugu wa kiume wa karibu

Mwongozo huo wa Serikali ambao umekosolewa na Wanaharakati pia umetoa wito kwa wamiliki wa magari kukataa kuwapandisha Wanawake ambao hawajavaa Hijabu

Hatua hii pia inafuatana na amri iliyowekwa ya wanawake kutofanya kazi katika sekta za wazi huku wasichana wakizuiwa kwenda shule za upilI

Mwongozo huu mpya unaozunguka katika mitandao ya kijamii umewataka wananchi wote wa Taliban kutosikiliza muziki katika magari yao

Wiki chache zilizopita pia Wizara husika ilizuia vituo vya habari vyote kutoweka maigizo, Tamthilia na maudhui ambayo wamehusika wanawake huku ikiwataka wanawake wote watangazaji wa televisheni kuvaa nikabu katika kazi

Shirika la Human Rights Watch limesema agizo hilo linawanyima Wanawake fursa ya kutembea kwa uhuru. Pia, linaondoa uwezekano wa kukimbia ikiwa wanafanyiwa vitendo vya Ukatili nyumbani

Simbachawene:Mwingira atafutwe na polisi haraka
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Disemba 27, 2021