Afarah Suleiman, Babati – Manyara.
Wanawake 20 kutoka katika vijiji vinne vya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara wamepewa elimu ya kuwajengea uwezo uwezo wa majukumu yao juu ya Sheria ya Ardhi no 5 ya mwaka 1999 na stadi za utetezi wa haki zao ili kumiliki Ardhi na Mali nyingine.
Elimu hiyo, wameipata katika Warsha iliyoandaliwa na shirika la COSITA, ambayo inalenga kuwakwamua Wanawake kujitambua wao wenyewe katika kumiliki Ardhi na kuachana na Mila kandamizi ikiwemo mfumo dume.
Afisa Mradi na mtoa mada kutoka katika shirika hilo, Paul John alisema Wanawake nchini wanatakiwa kupata haki zao kwa kuwa ndio wanaofanyakazi nyingi za kujenga uchumi wa familia, huku michango yao ikiwa haionekani wala kutambulika katika kaya na jamii kiujumla.
Kwa upande wao, baadhi ya wanawake hao walisema mafunzo hayo yataasaidia katika ufahamu na wataenda kuwafundisha wanawake wenzao walio vijijini, hasa katika maswala ya Mila kandamizi, mirathi, namna ya kumiliki Ardhi na jinsi ya kumtumia Mali zao.