Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Idadi ya watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA)  Dkt. Wilfred Ochan,  amewahimiza wanawake kutoa hamasa  kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi la Sensa ya watu na makazi litakalofanyika Agosti  mwaka huu.

Ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam  katika warsha ya  siku moja  ya mafunzo maalumu kwa wanahabari yaliyoandaliwa na UNFPA  kwa lengo la kuwajengea uelewa Wanahabari kuhusu zoezi la sensa la mwaka huu na kufafanua kuwa wanawake wana mchango mkubwa katika jamii hivyo wanapaswa kutumiwa ipasavyo katika kufikisha ujumbe wa sensa kwa jamii.

Ameongeza kuwa, kuelekea siku ya wanawake Duniani lengo  la maendeleo endelevu SDGs namba 5 limelenga kufanikisha usawa kijinsia na kuwawezesha wanawake  na wasichana kwa kutambua na kuthamini mchango wa wanawake na kazi zao majumbani kupitia mgawanyo wa majukumu ya kijamii miundombinu na sera za kutetea jamii na kupata mgawanyo sawa wa majukumu katika familia na ngazi ya Taifa.

“Kila mwaka ifikapo Machi 8, Umoja wa Mataifa ,Serikali na wadau wa maendeleo ya kijinsia tunaadhimisha siku hiyo ambayo kwa mwaka huu kauli mbiu yake ni “Usawa wa Kijinsia wa Leo kwa kesho endelevu”, kwa Tanzania kauli mbiu ni kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu,tujitokeze kuhesabiwa” amesema Dkt. Wilfred Ochan.

Naye Afisa Mawasiliano wa UNFPA  amewasihi Waandshiwa habari kutoa elimu na kuwahimiza  wanchi kujitokeza katika zoezi la Sensa litakapowadia kwani ni wajibu na haki kwa katika mstakabali wa maendeleo ya Jamii na Serikali.

Ajiua kwa kukimbia tuhuma za mauaji
Rais ateta na Baraza la Mawaziri