Nchini Sri Lanka serikali imefanya marekebisho ya sheria ya mwaka 1995 na kuruhusu wanawake waliotimiza umri wa miaka 18 kununua pombe na kunywa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka 60.

Serikali imesema imefanya marekebisho hayo ya sharia ambayo ilikuwa inawakatza wanawake kunywa pombe wala kufanya kazi katika sehemu za starehe za uuzaji wa pombe.

Marekebisho hayo ya sheria, ambayo yametangazwa Jumatano, yana maana kwamba wanawake wataruhusiwa kufanya kazi katika maduka na sehemu zinazouzwa pombe bila kuhitaji kuwa na kibali.

Wanawake wengi wamefurahia mabadiliko hayo na kutoa shukrani kwa serikali ya nchi hiyo. Kwenye sheria mpya iliyotangazwa na waziri wa fedha Mangala Samaraweera wanawake hawatahitaji ruhusa kutoka kwa kamishna wa forodha kufanya kazi au kunywa pombe katika maeneo yaliyoidhinishwa, ikiwa ni pamoja na baa.

Pombe ni kinywaji kizuri kama kitaweza kutumika kwa adabu, ila ni hatari kwa afya yako na watu wanaokuzunguka kama kitatumika bila ustaarabu, ndio maana wahenga husema pombe sio chai.

Kwa Tanzania natamani sheria hiyo ipitishwe ya kukataza kutumia pombe hasa kwa jinsia ya kike, kwani ni kinywaji ambacho huchochea madudu mengi na kumdhalilisha mwanamke na kumpa ujasiri wa kufanya vitu ambavyo mtu mwenye akili timamu hawezi kuvifanya.

Naiomba Serikali iweke kiwango cha unywaji pombe kwa wanawake ili kulinda heshima ya kina mama hasa wale wanaojisahau na kunywa bila kiasi.

 

Tatizo la rushwa ya ngono vyuoni kushughulikiwa vikali
Live Zanzibar: Sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar