Nchi za kiafrika, zimetakiwa kuongeza ushiriki wa Wanawake katika majukwaa ya maamuzi ikiwa ni moja ya njia za kuelekea kwenye usawa wa kijinsia.

Wito huo, umetolewa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima wakati wa ufunguzi wa mkutano wa AWLO jijini Arusha akisema moja ya kikwazo cha kufikia usawa wa kijinsia ni pamoja na Wanawake wengi kutopata nafasi ya kujiendeleza kielimu.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima.

Amesema, ni vyema kuongeza fursa sawa za kupata elimu kwa jinsia zote, ili kufikia malengo ya usawa wa kijinsia barani Afrika.

Aidha, Dkt. Gwajima pia ameongeza kuwa jamii yenye uchumi imara inaweza kutoa fursa sawa kwa jinsia zote katika elimu, biashara na fursa mbalimbali  zilizopo.

Asimulia jinsi alivyopata vitu vyake vilivyoibwa
Ruvu Shooting hatarini kupigwa bei