Zaidi ya Wanawake na Wasichana milioni 68 wapo kwenye hatari ya kukeketwa Duniani, wakati idadi barani Afrika ikiwa ni zaidi ya millioni 50. Kiwango ambacho kinaonyesha haja ya kufanya mabadiliko katika nchi za Afrika.

Hayo yamebainika katika mkutano wa pili wa kimataifa kuhusu kutokomeza ukeketaji wa wanawake, uliofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo Wadau wamesema utolewaji kwa mapana wa elimu kuhusu madhara ya ukeketaji ndiyo suluhisho sahihi litakalotokomeza vitendo hivyo barani Afrika.

Katika kikao hicho, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima aliwataka wadau kushirikiana na viongozi wa kimila, kidini, taasisi zisizo za kiserikali na jamii kuungana pamoja katika kutafuta suluhisho la kudumu la ukeketaji barani Afrika na duniani kwa ujumla.

Mkutano huo ambao ulikuwa na kauli mbiu “Mabadiliko katika kizazi kimoja kwenda kingine ni muhimu katika kutokomeza vitendo vya ukeketaji” umehudhuriwa na mataifa wanachama wa Umoja wa Afrika ikiwemo Misri, Ethiopia, Gambia, Ghana pamoja na nchi kutoka mabara mengine.

Kombe la Dunia 2034 lanukia Saudi Arabia
Alphonso Davies kuzigombanisha Man City, Real Madrid