Wanawake wengi miaka ya karibuni wanakabiliwa na tatizo linalofanana la kuwa na tumbo kubwa au kwa maneno mengine kitambi.

Kisayansi kitambi husababishwa na mlundikano wa mafuta sehemu ya chini ya tumbo na  mtu  kuonekana kama ana tumbo kubwa au kuhisi labda ni ujauzito kumbe ni ujazo mkubwa wa  mafuta tumboni.

Kwa ujumla ni vigumu sana kupunguza tumbo la namna hii, tutaangalia  visababishi vya tatizo hili, japokuwa dawa za asili zinazoweza kuondoa tatizo hilo na aina ya maisha unayotakiwa kuishi ili ufanikiwe kirahisi zaidi bila kukuachia madhara mengine yoyote.

Tatizo hili mara zote husababishwa na ulaji wa Vyakula feki (Junk food), Kutumia vyakula vya wanga kupita kiasi, Kutokunywa maji ya kutosha kila siku, Kula chakula kizito muda mchache kabla ya kwenda kulala au Kukaa masaa mengi kwenye kiti, Kutokujishughulisha na mazoezi, Mfadhaiko (stress), Kula wali kila siku, Ugali wa sembe, Kula vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi (chipsi, maandazi, nk)

Hivyo madaktari wanashauri kwa mtu aliyekumbwa na janga hili la kuwa na kitambi anashauriwa ale vyakula vinavyosaidia kupunguza mafuta mwilini, vyakula hivyo ni kama;

Asali na limau, maji ya uvuguvugu lita 1 ambapo hushauriwa kunywa asubuhi  tumbo likiwa tupu, hii husaidia kusafisha mwili na kuondoa mafuta yasiyohitajika mwilini.

Tumia Mdalasini, kitunguu swaumu, kunywa juisi ya limau, parachichi moja kwa siku na kula maharage  hufanya kazi ya kuchoma mafuta mwilini.

Tikiti maji lina asilimia 82 za maji  hivyo hufanya tumbo lako kutokuwa na njaa ya kuhitaji chakula, tikiti maji lina vitamini C ambayo ni muhimu kwa afya bora, fanya jitihada za kula tikiti kila siku.

Tumia tango lina asilimia 96 za maji na asilimia zinazobaki ni nishati. Tumia kachumbali yenye tango ndani yake kila siku au kula tu tango moja kila siku ili kupunguza mafuta tumboni kwa haraka.

 

 

 

 

 

 

Magazeti ya Tanzania leo Juni 27, 2017
Mfahamu Ed Sheeran nje ya uimbaji