Watu wanne (Waumini wa Kanisa la Good News International Church), wamekutwa wamefariki na wengine zaidi ya kumi wamelazwa hospitali ya Kaunti ya Pwani ya Kilifi nchini Kenya, baada ya kuokolewa wakisema wanasubiri mwisho wa dunia unaokaribia.
Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi nchini humo, imesema watu hao lilipatikana katika msitu walimokuwa wakiishi kwa siku kadhaa baada ya Mhubiri wa eneo hilo kuwataka kufunga huku wakingoja kukutana na Yesu.
Mmoja wa waathiriwa wa tukio hilo. Picha ya Markion Kithi/Standard.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, watu 11 waliokolewa na sita kati yao walikuwa wamedhoofika wakiwa katika hali mbaya ya kiafya huku msako wa kuwatafuta wanachama zaidi wa kundi hilo ukiendelea kutokana na taarifa kuwa wengine walikuwa bado msituni.
Kanisa hilo la Good News International Church linaongozwa na Mchungaji, Paul Mackenzie ambaye amekuwa alikamatwa na Polisi kwa madai ya kuwataka waumini wake kufa njaa ili kufika mbinguni kwa kasi ambaye yuko huru kwa dhamana baada ya kushtakiwa mwezi uliopita kuhusu kifo cha watoto wawili ambao wazazi wao ni miongoni mwa wafuasi wake.