Wachezaji wanne wa Klabu ya Simba SC wamekubali kuongeza mikataba na kuendelea kusalia klabuni hapo.

Wachezaji hao waliokubali kusalia viunga vya Msimbazi ni Hassan Dilunga, Said Ndemla na Deo Kanda waliyoongeza mikataba ya miaka miwili kila mmoja na Muivory Coast Pasco Wawa aliyeongeza mkataba wa mwaka mmoja.

Taarifa zaidi zinasema kuwa timu ya Simba SC bado ipo kwenye mazungumzo na viungo Mzamiru Yassin pamoja na Sharaf Shiboub ili nao waweze kuongeza mikataba.

Ikumbukwe kuwa Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Congo, Deo Kanda alikuwa akihudumu Klabuni hapo kwa mkopo akitokea TP Mazembe ya nchini Congo.

Sikukuu ya Eid: Benki ya Exim yatoa msaada kwa watoto yatima mikoa minne
Mosimane azima kelele za kuikacha Sundowns

Comments

comments