Klabu ya Dodoma Jiji, imeamua kuingia tena sokoni kusaka viungo wanne kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chake baada ya kugundua kuna baadhi ya mapungufu kwenye mechi zake za kirafiki.

Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Kassim Liogope, amesema baada ya kucheza mechi kadhaa za kirafiki wamegundua baadhi ya mapungufu kwenye kikosi, hivyo wanatakiwa kuyarekebisha haraka sana kabla ya kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Hata msimu uliopita tulikuwa na tatizo kama hili, tunachofanya ni kuongeza watu eneo la kiungo na hao tutawapa majukumu, kazi yao itakuwa ni kutengeneza nafasi nyingi,”

“Hizi wiki mbili tulizokaa Iringa zimetunufaisha kwa sababu wachezaji wanaonekana kupokea vizuri mafunzo, tulicheza mechi za kirafiki ambazo zimetufanya tuone kuna baadhi ya mapungufu kwa hiyo sasa tunajitahidi kuyaziba ili kuhakikisha tukitoka hapa tupo kamili kwa mapambano,” amesema Liogope.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 9, 2023
Goran Copnovic azionya Simba SC, Young Africans