Raia wawili raia wa Marekani na mbwa wao wawili wameokolewa na jeshi la wanamaji la Marekani baada ya kukaa baharini karibu miezi mitano huku chombo chao kikielea katika bahari ya Pacific kwa mujibu wa maafisa jeshi hilo.

Jennifer Appel na Tasha Fuiaba walianza safari yao huko Hawaii wakielekea Tahiti wakati wakiendelea na safari yao injini ya mashua yao ilipata hitilafu kutokana na hali mbaya ya hewa.

Aidha, baada ya injini hiyo kupata hitilafu, mashua yao iliendelea kuelea baharini katika umbali wa kilomita 1,500 kusini mashariki mwa Japan,na baadaye kuokolewa baada ya meli za uvuvi kutoa taarifa katika katika jeshi la maji la Marekani.

Wanawake hao walianza safari yao mwezi Mei na walifikiri kuwa wangefika nchi kavu wakielea kwa nguvu za upepo, lakini ikawa kinyume na walichotegemea mpaka pale walipookolewa na jeshi la wanamaji la Marekani.

Jeshi la Marekani limesema kuwa wanawakake hao waliendelea kutuma ishara kila siku lakini ishara hizo hazikuoneka kwa sababu walikuwa mbali na vyombo vingine vya majini au karibu na vituo viivyo ardhini.

Hata hivyo, Oktoba 24, meli ya uvuvi ya Taiwan ilitambua mashua hiyo baharini na kuzijulisha mamlaka za Marekani katika kisiwa cha Guam kilichopo Japan., ambapo Meli ya USS Ashland ambayo ilikuwa eneo hilo iliwasili kesho yake kuwakoa mabaharia hao kutoka Honolulu pamoja na mbwa wao.

Mpina: Nitang'atuka nafasi ya Uwaziri kama nitashindwa
Video: 'Bado mwezi mmoja puto la Seth lipasuke' Wakili, Mambo ya nje yamchefua JPM