Serikali imesema kuwa ipo katika mchakato wa kuandaa sheria ambayo itaondoa utaratibu wa kulipa kodi ya pango kwa miezi sita au mwaka kwa nyumba za makazi ili kuweza luwapatia unafuu wananchi.

Hayo yamesemwa bungeni na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angeline Mabula wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa viti maalum Halima Bulembo aliyetaka kujua ni lini serikali itatunga sheria itakayompa nafasi mpangaji kulipa kodi ya mwezi mmoja na si miezi sita au mwaka kama ilivyosasa.

“Wizara tayari imeshaliona hilo na tupo kwenye mchakato wa kuanzisha mamlaka itakayosimamia masuala yote ya nyumba, katika sheria inayoandaliwa kwaajili ya kuletwa bungeni imeangalia ukomo wa kutoa kodi hivyo hiyo ya miezi sita haitakuwepo,” amesema Mabula

Aidha, Mabula amesema kuwa baada ya sheria hiyo kupitishwa kodi itakuwa inatolewa kwa mwezi mmoja mmoja, huku wakati huo mpangaji atalazimika kutoa amana ya miezi mitatu kwaajili ya mambo mengine yanayoweza kujitokeza.

Hata hivyo, Halima Bulembo ameuliza swali hilo kwa kuzingatia malalamiko ya vijana wengi ambao ni zaidi ya asilimia 55 nchini kuwa wanashindwa kutimiza malengo yao kutokana na gharama kubwa za kulipa kodi kwenye nyumba za makazi kuwa kubwa huku wamiliki wakiomba kulipwa kwa miezi sita hadi mwaka mmoja.

Jamal Malinzi, Selestine Mwesigwa mambo bado magumu
Kaburu, Aveva warejeshwa rumande hadi Novemba 30