Kwa mara ya kwanza, wanaume wawili wapenzi wa jinsia moja (mashoga) nchini Afrika Kusini wametajwa kupata mapacha watatu kwa njia siyokuwa ya kawaida wakikutanisha vinasaba vyao (DNA).

Kwamujibu wa SkyNews, wawili hao ambao walikuwa wanahangaika namna ya kupata mtoto mwenye damu yao, walikutana na mwanamke mmoja nchini Afrika Kusini kwenye sherehe ya marafiki wa mwanariadha Oscar Pistorius baada ya kesi ya mwanariadha hyo.

Imeelezwa kuwa baada ya mazungumzo, walifanikiwa kumshawishi mwanaumke huyo kubeba ujauzito wao kwa kutumia mchanganyiko wa wawili hao.

Mwanamke huyo amefanikiwa kupata mapacha hao watatu na kwamba wawili kati yao ni mapacha wanaofanana. DNA imeonesha watoto hao ni wawili hao.

Simba SC Yawasilisha Barua Ya Madai Ya Hassan Kessy
Mrema ataka Chadema wasibembelezwe