Lydia Mollel – Morogoro.

Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara, imewaagiza Wataalam wanaoshughulika na usajili wa Leseni za Biashara, Taasisi na Makampuni mbalimbali nchini, kutatua changamoto za Wafanyabiashara licha ya uwepo wa mikinzano ya sheria kati ya taasisi za usajili na za udhibiti.

Agizo hili, limetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah wakati wa kikao kazi kilichodumu ndani ya siku tatu kati ya BRELA na taasisi za Udhibiti, kilichofanyika Mkoani Morogoro.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa BRELA, Godfrey Nyaisa amesema kutokana na mabadiliko ya teknolojia kwa sasa wanaitaji sheria zitakazowasaidia Wananchi huku Mkurugenzi wa Udhibiti ubora shirika la viwango Tanzania – TBS, Lazaro Masalanga akiainisha mapendekezo yaliyoyotewa na wadau.

Amesema, mapendekezo hao yanataka baadhi ya sheria, kanuni na taratibu kufanyiwa marekebisho huku sheria moja ya wapo ikiwa ni ya leseni ya biashara kifungu cha 14 1B, ili kuruhusu baadhi ya biashara zinazodhibitiwa kupewa leseni kabla ya vibali kutoka Mamlaka ya Uthibiti kwa kuzingatia aina ya biashara na huduma.

Sendiga aukubali uwekezaji Kiwanda cha kuzalisha Vinywaji
Watafiti wapimwe kwa ubora wa kazi zao - Prof. Mkenda