Baada ya kutolewa kwa ripoti ya kamati mbili za bunge kuhusu biashara ya madini ya almasi na Tanzanite, vigogo wote waliohusika katika kuisababishia hasara serikali wanakabiliwa na hatari ya kufilisiwa mali zote wanazomiliki.

Hali hiyo imejidhihirisha mara baada ya Serikali kumtaka Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Mganga Bisawalo kuhakikisha ushahidi unapatikana na wahusika wanafikishwa mbele ya mkono wa sheria.

Aidha, agizo hilo limetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango wakati wa kukabidhiwa kwa mzigo wa madini ya almasi uliokamatwa Septemba Mosi mwaka huu Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (JNIA).

“Hali ya taifa kuendelea kuibiwa haivumiliki hata kidogo katika kipindi hiki ambacho Serikali ingali inapambana kuhakikisha kuwa watanzania wananufaika na rasilimali zao, DPP hakikisha ushahidi unapatikana haraka zaidi ili sheria ichukue mkondo wake,”amesema Dkt. Mpango

 

Hata hivyo, Dkt. Mpango ameongeza kuwa wahusika hao wanatakiwa kuchunguzwa kwa kina na kufilisiwa mali zao ikibidi na watumishi wote walioshiriki mchakato wa usafirishaji wa vito, kuanzia wa sasa, walioacha kazi pia na waliostaafu.

 

 

IGP Sirro atoboa siri ya kukutana na viongozi wastaafu wa Polisi
Stoke City yaibana mbavu Man United