Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu amelielekeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), kufuatilia na kutoa adhabu kali kwa wanaopiga kelele za muziki bila taratibu kwenye maeneo ya makazi.

Zungu ametoa maelekezo hayo wakati wa kuhitimisha mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira hii leo Aprili 24, 2023 Bungeni jijini Dodoma.

Amesema, “makelele kwenye maeneo ya watu yanakera, watu wanaugua wazee wengi wanateseka sana na makelele ya muziki wala haina control yoyote kwahiyo NEMC mlifuatilie na mtoe adhabu kali kwa wanaokiuka taratibu za uchafuzi wa mazingira hasa kwenye makelele.”

Bunge hii leo limepitisha makadirio ya shilingi 54.1 Bilioni kwa ajili ya matumizi kwa mwaka 2023/24.

Man Utd wamfungia kazi Victor Osimhen
Bodaboda Dar Wapewa Vifaa vya Usalama