Mtandao maarufu wa WhatsApp umepiga marufuku watu walio chini ya umri wa miaka 16 kutumia mtandao huo, kwenye nchi za Umoja wa Ulaya.
Kabla ya hapo watumiaji walitakiwa kuwa na umri wa miaka 13, lakini sasa watumiaji ni lazima wawe na miaka 16 na kuendelea kulingana na utaratibu mpya wa kulinda taarifa binafsi Barani humo.
Aidha, mtandao huo ambao unamilikiwa na mtandao mkubwa wa facebook, utawauliza watumiaji kuthibitisha umri wao watakapo jisajili kuanzia mwezi ujao mwaka huu.
Hata hivyo, kutokana na hilo WhatsApp utakuwa mtandao wa kijamii wa tano kuhitaji umri maalum ili kuweza kuutumia, ikiwemo Facebook, Snapchat, Instagram na YouTube.
-
Jacob Zuma atangaza ndoa kwa mara ya 7
-
Wafuasi wa vyama vya upinzani waendelea na maandamano nchini Madagascar
-
Marekani yashutumiwa kwa ongezeko kubwa la uhalifu dhidi ya Waislam