Kikosi cha Medeama SC ina hali ngumu ya ukata inayowakabili. Inaonekana mambo ni magumu hadi sasa hawana uhakika wa kufika Lubumbashi nchini DR Congo ili kuwavaa TP Mazembe Juni 19.

Katika michuano ya Kombe la Shirikisho, Medeama ya Ghana iko katika kundi moja pia na Yanga na Mo Bejaia.

Imeelezwa Medema wamekuwa wakifanya kila juhudi kupata fedha lakini wamegonga mamba na huenda fedha kutoka Shirikisho la Soka Afrika (Caf) ndiyo zimebaki kuwa tegemeo kwao.

Kawaida Caf hutoa kiasi cha fedha kwa kila hatua ya michuano hiyo na Medeama wanaitegemea fedha hiyo ingawa wanaonekana kuwa na wakati mgumu katika suala la maandalizi.

Hata hivyo, bado habari hizo hazijathibitishwa na msemaji au ofisa wa juu wa klabu hiyo. Ingawa ilielezwa mmoja wa viongozi wake, Benjamin Kessie.

Carlos Dunga Atupiwa Virago
Video: Mbunge Bahati ameitaka Serikali kuwatibia bure Wanawake wenye tatizo la Fistula