Upinzani nchini Sudan umetangaza kufanya kampeni ya uasi wa kiraia wa nchi nzima kuanzia Jumapili (09.06.2019) hadi pale baraza la kijeshi la mpito litakapokabidhi madaraka kwa serikali ya kiraia.

Tangazo hilo limetolewa na chama cha wanataaluma wa Sudan SPA, ambacho awali kilianzisha maandamano dhidi ya kiongozi wa muda mrefu, Omar al-Bashir aliyeondolewa madarakani.

Maandamano hayo yanakuja siku chache baada ya jeshi kuwashambulia waandamanaji na kusababisha watu kadhaa kupoteza maisha jijini Khartoum na hivyo kuvunja matumaini ya makabidhiano ya kidemokasia ya madaraka.

“Vuguvugu la uasi wa kiraia litaanza Jumapili na kukoma tu pale serikali ya kiraia itakapojitangaza yenyewe kupitia televisheni ya taifa”, imesema sehemu ya taarifa ya chama cha wanataaluma wa Sudan SPA.

Aidha, tamko lao linakuja siku moja baada ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed kukutana kwa nyakati tofauti na Majenerali wanaotawala na viongozi wa waandamanaji katika juhudi za kufufua mazungumzo ambayo yalikaribia kuvunjika baada ya waandamanaji waliopiga kambi nje ya makao makuu ya jeshi kutawanywa siku ya Jumatatu.

Hata hivyo, chama cha wanataaluma wa Sudan ambacho kiliongoza maandamano yaliyomuondoa Bashir, kimesema kinakubaliana na usuluhishi wa waziri mkuu Ahmed lakini kikatoa masharti kabla ya kurejea meza ya mazungumzo.

Video: TRA kaa la moto, Sababu tisa zang'oa mawaziri 15
Video: RC Makonda awaonya wabunge wa Dar, 'Msipofanya ziara 2020 mtaisikia tu'

Comments

comments