Kundi la maseneta wa Italia wametoa wito kwa watengenezaji wa Pizza kupasi mitihani yao ili kuboresha viwango vya uundaji wa mlo huo.

Wabunge ishirini na wawili katika bunge la juu waliwasilisha mswada, ambao ukiidhinishwa kuwa sheria,itapendekeza kusajiliwa kwa taaluma maalum ya pizzaoli-wapishi wa pizza.                                                                                                                                       Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na shirika la habari la Rai,Taaluma hiyo itajumuisha kozi zitakazosomewa kwa jumla ya saa mia moja ishirini itakayo muezesha mwanafunzi kufuzu kwa Diploma   .

Katika mapendekezo hayo , wale wanaopania kuwa Pizzaoli wanastahili kupasi mitihani wa kinadharia na wa kivitendo baada ya kusomea sayansi ya chakula,usafi na lugha za kigeni msisitizo zaidi ukipewa lugha ya kiingereza.                                        Wale ambao wamekuwa wakitengeneza kwa angalau miaka kumi au zaidi,ambao wanaweza kuungana katika kikundi cha watu wanne moja kwa moja watatambuliwa “master Pizzaoli”

Maseneta hao wanasema karibu pizza milioni nne huliwa kila siku Nchini Italia, hivyo basi ipo haja ya kuandaa pizza inayofikia viwango vya juu.

Italia ina jukumu la kudumisha hadhi yake kwa kuwa inafahamika kwa uundaaji wa pizza za aina yake duniani.

Senata Bartolomeo Amidei, alisema “kwa kuzingatia hilo hii ni nafasi ya kujiboresha na watengenezaji wa pizza wanastahili kutilia maanani pendekezo hilo”.

Pendekezo hilo tayari limepata uungwaji mkono kutoka kwa shirika la Genuine Neapolitan Pizza na mtengenezaji mmoja wa pizza amemwambia Il Messaggero kuwa mswada huo ni “tendo la haki” kwa sababu inatambua kile yeye na wenzake ni “mafundi”.

Sekta Ya Filamu za Ngono Yaomba Msamaha Japan
Mwanasiasa 'atingishwa' baada ya kujinadi kwa kula nyama ya Simba, twiga