Klabu ya Al-Nassr imedhamiria kumsajili Mlinda Lango kutoka nchini Cameroon na klabu ya Ajax ya Uholanzi Andre Onana, katika dirisha hili.

Mlinda LAngo huyo mwenye umri wa miaka 27, ambaye pia anawindwa na Manchester United inadaiwa amewekewa ofa ya mshahara mara mbili zaidi ya ule anaopata Inter, lakini hajafanya uamuzi ikiwa atatua Saudia Arabia au atabaki Ulaya.

Nyota huyu huduma yake imetuma ofa Inter Milan ili kuipata huduma ya kipa wa timu hiyo na inahitajika Man United kwa sababu huenda akaziba pengo la David De Gea vizuri.

Onana ambaye msimu uliopita aliisaidia Inter Milan kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2027.

Msimu uliopita alicheza mechi 41 za michuano yote, akaruhusu mabao 36 na mechi 19 alimaliza bila kufungwa.

Mlinda Lango Andre Onana

Ikiwa dili hilo litakamilika Onana atakwenda kucheza timu moja na Cristiano Ronaldo ingawa uhusiano wake na kocha wa Man U, Erik Ten Hag huenda umfanya atue Old Trafford.

Geita Gold FC yabisha hodi Zanzibar
Jonas Mkude atumika kuitisha Simba SC