Boniface Gideon – TANGA.
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amekabidhi Vitendea kazi vya ujasiriamali, vifaa tiba na vitendanishi katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Tanga, Bombo kwa Vijana waliokuwa wakipata huduma ya methadone na kuhitimu, ili waweze kubadilisha maisha yao watakaporudi uraiani.
Akizumza baada ya kukabidhi vifaa hivyo, Ummy amesema vitawasaidia kujikwamua kiuchumi na kuweza kufanya shughuli za kujiingizia kipato halali na hivyo kuachana na kufikiria kurudi kwenye matumizi ya dawa hizo.
Vifaa walivyokabidhiwa vifaa kwa ajili ya kutenegeneza madirisha ya milango seti mbili vyenye thamani ya Milioni 38 na vyerahani 10 vyenye thamani ya Milioni 48 pia watakwenda kutatafuta shule ambazo watakuwa wakiwashonea wanafunzi kila mwaka.
Amesema watakabidhi mashine mbili za matofali kwa siku zenye thamani ya Milioni 70 ambapo alimtaka Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga tenda ya kwanza oda ipewe watu wa MAT ili kuweza kulisaidia kundi la vijana waliokuwa wakitumia dawa zaa kulevya, ili kuwainua kiuchumi na washiriki kwenye shughuli za kimaendeleo na hatimaye wasirudi kule walipotoka katika matumizi ya dawa za kulevya.
“Ndugu zangu vijana wa Tanga ambao bado hamjaingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya msiingie huko lakini nafurahi kuna taasisi zinaelimisha vijana wa Tanga naomba waongeze nguvu katika hili ili kuwaepushga vijana na utumiaji,” alisema Ummy.
Aidha, alizitaka Taasisi ambazo zimekuwa zikitoa elimu kwa vijana viwafikie vijana kwenye shule za Msingi na Sekondari kuwahamasisha wasijiingize kwenye matumizi ya dawa za kulevya huku akiwaasa waraibu wanaotumia dawa za kupunguza makali ya dawa za kulevya kuhakikisha hawakatishi matibabu mpaka watakapoambiwa wapo sawa.
“Tunaomba nyie muwe mabalolozi tuwe na mpango wa kupita kwenye shule za Msingi na Sekondari na tunaandaa mambo mbalimbali kuhakikisha tunatoa elimu kwa wanafunzi, kuna ambao mnapata matibabu na kuamua kuacha wenyewe hapana msikatishe matibabu mpaka mtakapoambiwa mpo sawa lakini pia niwatake vijana waliopo majumbani tuache kujiingiza kwenye matumizi ya dawa hizi,” alissisitiza.