Mashindano ya Mrembo wa Dunia mwaka huu yanatarajiwa kufanyika Sanya nchini China ambapo mrembo wa dunia mwaka 2017-2018 kutoka India, Manushi Chhillar atakuwa anakabidhi taji hilo kwa mreambo mpya wa mwaka 2018/2019.

Mashindano hayo yatakuwa ya 68 tangu kuanzishwa kwake na mwaka huu yatafanyika Disemba 8 ambapo mpaka sasa nchi 85 zitakazoshiriki zimeshapata washiriki wake huku nchi nyingine zikiwa bado.

Aidha, mpaka ifikapo Oktoba 8 mwaka huu nchi 25 zilizobaki zinatakiwa ziwe zimeshawasilisha majina ya washiriki wao.

Kutoka Afrika hawa ni moja ya washiriki watakao tuwakilisha katika kinyanganyiro hicho;

Thulisa Keyi (Afrika Kusini)

Huyu ni mrembo kutoka Afrika Kusini, ambaye alishika namba moja katika mchuano nchini humo akiwaburuza warembo wengine na kuibuka mshindi.

Mashindano ya Umiss Afrika Kusini yamefanyika mwishoni mwa mwezi Mei kwenye ukumbi wa Sun Arena katika Jengo la Time Square, Pretoria ambapo mrembo Thulisa aliwaburuza warembo 28 huku Bonang Matheba akiwa mwongozaji wa shindano hilo.

Musa Kalaluka (Zambia)

Mrembo kutoka lisaka ndiye atakaye wakilisha Zambia katika mashindano ya Dunia yatakayofanyika Sanya nchini China huku ambapo akiwabwaga warembo wenzanke 21 katika mashindano ya nchini kwao.

Tiwonge Munthali (Malawi)

Mashindano ya Miss Malawi yalifanyika siku moja na ya Tanzania ambopo Mrembo Tiwonge Munthali ndiye aliyeibuka kidedea baada ya kuwashinda warembo wenzanke 14.

Belinda Potts (Zimbabwe)

Shindano la kumsaka Mrembo nchini Zimbabwe lilifanyika siku ya Jumamosi kama ilivyo fanywa na Tanzania, Malawi na nchi nyingine ambapo nchini humo mrembo Belandina Potts mwenye umri wa miaka 21 ndiye aliyeshinda taji la Miss Zimbabwe.

Lilian Iradukunda (Rwanda)

Llian Iradukunda ndiye aliye ibuka mshindi katika shindano la Miss Rwanda lililo fanyika mapema mwaka huu huku akiwabwaga walimbwende wenzake 20 na kuchukua nafasi ya ndugu yake Elsa Iradukunda aliyekuwa Miss Rwanda mwaka uliopita.

Queen Elizabeth Makune (Tanzania)

Nchini Tanzania Queen Elizabeth Makune ndiye aliibuka mshindi wa Miss Tanzania ambaye ataiwakilisha Tanzania katika mshindano ya Dunia nchini China.

Final Galaiya (Kenya)

Kinyang’anyiro cha Umiss kilifanyika pia siku ya Jumamosi iliyopita huko Westlands, Nairobi nchini Kenya ambapo Finali Galaiya ndiye atakayeiwakilisha nchi yake nchini China.

Quinn Abenakyo (Uganda)

Mshindi katika shindano  la Miss Uganda ni Quinn Abenakyo, mrembo mwenye miaka 22, aliyefanikiwa kuwashinda warembo 21 waoshiriki wakitoka majiji mbalimbali ya taifa hilo. Huku jaji mkuu wa shindano hilo akiwa ni Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.

Kubenea amkana Waitara, apiga teke barua ya kujiuzulu
CCM yaongoza kuwa na wasomi wengi bungeni