Wasaf noiri 80 kati ya 180 waliowekwa karantini kwenye Mpaka wa Isongole unaotenganisha Tanzania na Malawi na Tunduma wilayani Momba (Tanzania-Zambia) wameruhusiwa kuendelea na safari zao baada ya kumaliza siku 14 walizowekwa kwaajili ya uangalizi kama wanamaambukizi ya ugonjwa wa Corona.
Mganga mkuu wa Mkoa wa Songwe Dk Hamd Nyembea amesema katika kuchukua tahadhari ya Corona kuanzia machi 23 hadi April 14 tayari mkoa wa Songwe umeshawaweka karantini wasafiri 180 waliokuwa wakitokea nchi mbalimbali kupitia malawi na Zambia kuja Tanzania ambapo katika mpka wa tunduma waliwekwa karantini wasafiri 178 na mpaka wa Isongela watu wawili.
”chagamoto kubwa tuliokuwa tunakabiliana nayo ni wale wasafiri waliokuwa wakitoka nchi mbalimbali kwani kwetu sisi tuliona ni hatari, Songwe nasi tulichukua hatua kwa kufuata maagizo ya serikali kupitia wizara ya afya na kuwaweka karantini wasafiri karantini siku 14 na tmewaruhusu”amesema Dk Hamd Nyembea
Mganga mkuu huyo amesema mpaka kufikia sasa idadi ya wasafiri waliokuwa wakiingia kutoka nchi hizo kupitia mipaka ya Tunduma na Isongole imepungua ikilinganishwa na idadi ya waliokuwepo karantini na mkoa huo umeimarisha vipimo na upimaji lengo ni kulinda Tanzania.
Aidha amewaomba watanzania kutii kukaa karantini kwani kukaa humo sio adhabu kama ambavyo watu wengine wanatafsiri bali ni utaratibu amabo unalenga kuhakikisha Tanzania na familia inakuwa salama