Rais wa shirikisho la filamu Tanzania Elius Mjata afafanua dhamira ya serikali kupitia wizara ya Sanaa na Utamaduni kuamua kutoa mkopo kwa wasanii wa sanaa mbali mbali nchini ikiwamo wasanii wa filamu ili kuwawezesha kujiendeleza na kufikia mafanikio kupitia kazi zao za kibunifu.

Kufuatia hatua hiyo ya serikali Mjata ameweka bayana vigezo stahiki anavyopaswa kuwanavyo msanii anayehitaji kuchukua mkopo kwa ajili ya kujiendeleza ikiwa ni pamoja na kutoa angalizo kwa yeyote atakayechukua mkopo huo na kuutumia kinyume cha kusudio au kukiuka kanuni na taratibu zilizowekwa na wizara.

“Watu wengi Tanzania wanavipaji na wanamawazo mazuri lakini ili uendeleze kile kipaji au uendeleze stori yako ya filamu lazima uwe na fedha na ili uwe na fedha kama huna utaenda kukopa na kwenye mabenki tulikuwa hatukopesheki kwanza.

Kwa sababu lazima kwanza mtu awe na shamba, awe na nyumba, awe na kiwanja, sasa mtu kama anashindwa tu kwa vitu vidogo hawezi kuwa na kiwanja hawezi kuwa na nyumba, unaweza kuona kuwa hilo wazo lake lazima linashinwa kuendelea, kwa sababu mtu anakuwa hakopesheki wala hana sifa za kukopeshwa.

Lakini pia riba za kwenye taasisi zakifedha riba ni kubwa, na ndio maana serikali imekuja na utaratibu wa kukopesha bila riba yeyote, kwa hiyo ukikopa milioni ishirini utarudisha milioni ishirini”. amesema Mjata.

Aidha mjata amewashukuru viongozi wa shirikisho la filamu waliotangulia kabla yake na kuichonga barabara ya maendeleo ya tasnia ya filamu nchini, ambapo aweka wazi madhaifu machache yaliyosalia kwenye sekta ya filamu na namna ambayo kama Rais wa shirikisho hilo atahakikisha anakabiliana nalo ili kuboresha zaidi.

“Kila mtu sasa anatakiwa afuatilie lakini ni kwa wale tu ambao wako serious na kazi, wasije wakafikiria ni fedha ambazo zitaenda kuchukuliwa tu, halafu zitatumiwa tofauti na walivyoomba halafu wategemee serikali haitafuatilia, serikali lazima itafuatilia” ameongeza

Mjata ameyasema hayo kwenye mahojiano maalumu na Dar24 Media wakati wa uzinduzi wa platform ya usambazaji wa filamu Serena hotel jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma lililopita.

Mchengerwa ‘aongoza tukio’ utolewaji wa hundi

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Desemba 28, 2022
Mfumuko wa bei, uhaba wa chakula vyaathiri Watoto mil. 20