Mara baada ya mwanamuziki maarufu, Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego kuweka video katika ukurasa wake wa instagram akiwaponda wasanii kuwa na mabaunsa wa kuwalinda, msanii wa ‘bongo movie’ Duma amepingana na msanii huyo baada ya kuingia na mabaunsa usiku wa uzinduzi wa filamu yake  Mlimanicity.

Duma amesema kuwa mabaunsa hao ni kwaajili ya usiku huo wa kihistoria lakini pia kuna watu ni wengi lolote linaweza kutokea ni kwaajili ya usalama tuu.

“Mabaunsa hawa wananilinda kwa ajili ya tukio hili kubwa na la kihistoria, nikaona sio mbaya nikaingia na watu wakani ‘support’ kwa namna moja au nyingine ni kitu kizuri lakini huwezi kujua watu wanaweza wakakuvamia kwa sababu hapa watu ni wengi na wengine wanaweza wasiwe wazuri kwa upande wangu”amesema duma.

Ney wa mitego kupitia ukurasa wake wa instagram aliandika  ”sasa hivi kutembea na mabaunsa imekuwa ‘fashion’ sio kama usalama wa mtu, maana naona hata ‘video queen’, wadangaji, DJ’s na wao wana mabaunsa, pia wasanii wengine hawana sababu ya kutembea na baunsa kwanza hawana hela”.

Kipenda cha video cha msanii huyo kilionekana kupedwa na mashabiki zake huku wengi wakitoa maoni yao na kimetazamwa zaidi ya mara 124,426 kwa muda mfupi zaidi.

 

Watumishi wa Ardhi ‘waliokacha’ Mafia kikaangoni
Video: Rais Magufuli akoleza moto, Wakuu wa mikoa hawa hatarini