Tanzania inaendelea kung’ara katika tasnia ya muziki Afrika ambapo hivi sasa ni nadra kulikosa jina la msanii wa Tanzania katika orodha ya tuzo kubwa zinazojumuisha wasanii wa Afrika.

Jana, Julai 20 yametangazwa majina ya washiriki wa tuzo za AFRIMMA zinazotolewa Oktoba 10, Dallas, Marekani na majina ya wasanii tisa wa wasanii wa Tanzania yamejumuishwa.

Wasanii hao ni Lady Jay Dee, Vannessa Mdee, Mrisho Mpoto, Khadija Kopa, Ommy Dimpoz, Ali Kiba na mtayarishaji wa muziki Sheddy Klever.

Mshindi wa tuzo za MTV/MAMA2015, Diamond Platinumz ameongoza kwa kutajwa katika vipengele takribani saba.

Bofya hapa kuangalia orodha kamili na kupiga kura:

Fahamu Vibweka Vya Aliyemrushia Noti Bandia Sepp Blatter
Ciara Ayapotezea Malalamiko Ya Future