Wasanii wa sanaa za ufundi Zanzibar, wameomba mradi wa TACIP uwafikie kwa haraka ili kuwasaidia kuondoa changamoto wanazo kabilina nazo katika kuendesha shughuli za sanaa na biashara kisiwani hapo.
Maombi hayo yametolewa na baadhi ya wasanii wa sanaa za Uchongaji na Uchoraji walipo zungumza na Dar24, na kueleza shauku waliyonayo ya kufikiwa na Mradi wa Utambuzi wa Wasanii wa Sanaa za Ufundi TACIP ili nawao weweze kutambulika.
“Sisi wachongaji hatutambuliki kabisa, tofauti hata na wenzetu Mafundi Gereji ambao hata wana mavazi yao yanayoweza kufanya watambulike, sisi tunaonekana mabishoo tu, bora utufikie mradi huu na sisi tutambulike.” Mahadi Mohamed aliongeza.
Miongoni mwa changamoto kubwa kwa wachoraji ni masoko, ambayo upande wa wachoraji waliopo eneo la forodhani wanatamani mradi wa TACIP ukawatatulie, “tukimaliza kuchora tunawauzia wenye maduka kwa bei ya chini sana, tuna tamani nasisi kuuza moja kwa moja kwa wataliI” aliongea kiswanta kiswanta moja ya wachoraji waeneo hilo.
Mradi huo wa Utambuzi wa Wasanii wa Sanaa za Ufundi ambao unaratibiwa na kampuni ya Data vision international kwa kushirikiana na (TAFCA) chini ya wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, unatarajia kuwafikia Wasanii wote Bara na Visiwani.