Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukombe mkoani Geita, hivi karibuni ililazimika kuahirisha kesi inayowakabili watu watano wanaotuhumiwa kulisha ng’ombe 454 kwenye eneo la hifadhi ya Taifa ya Kigosi baada ya watu wasiojulikana kufyatua risasi kadhaa wakilenga eneo la Mahakama.

Hakimu Mkazi Mwandamizi, Gabriel Kwirijila alikitaja kitendo hicho kama kitendo cha uoga kilichofanywa na watu wasiojulikana waliokuwa na nia ya kuvuruga zoezi hilo, katika eneo ambalo Mahakama ilihamia kwa ajili ya kutambua mifugo iliyotajwa kuhusika.

Hata hivyo, Polisi waliongezwa katika eneo hilo na kujibu mapigo. Risasi za polisi zilizoelekezwa kwa watu hao walioanza kushambulia ziliwakimbiza na kuwafanya watokomee kusikojulikana.

Baada ya muda mfupi, Mahakama ilirejea na kuendelea na zoezi la utambuzi wa mifugo husika huku Polisi 10 na askari wa hifadhi hiyo 35 wakiimarisha ulinzi.

Wakili wa Serikali, Mwasimba Hezron alieleza kuwa katika zoezi hilo, ng’ombe 139 kati ya 454 walitambuliwa.

 

 

 

 

Jonjo Shelvey: Sitaisaliti Newcastle Utd Hata Ikishuka Daraja
MADUDU YABAINIKA MADAI YA WATUMISHI