Wanandoa wametakiwa kufanya majadiliano ya mara kwa mara, kujua changamoto zinazowakabili katika ndoa zao na kutafuta suluhu ili kuondokana na msongo wa mawazo unaopelekea kutokea kwa vitendo vya ukatili.
Hayo yamesemwa na Polisi Kata wa Kata ya Mikumi Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Evodia Komba wakati alipokutana na wananchi maeneo ya Kidoma stendi ya Zamani.
Aidha, Mkaguzi Komba alitoa elimu juu ya Kampeni ya Siku 16 za kupinga ukatili na namna zitakavyosaidia kupunguza vitendo hivyo, utambulisho wa mradi wa ongea nao, madhara ya dawa za kuelevya pamoja na familia yangu haina mhalifu.
Wakati huohuo, Wananchi wa Kijiji cha Masheshe, Mkoani Kagera wamepewa elimu ya utoaji wa taarifa ya uhalifu na wahalifu iliyotolewa na Polisi kata wa Kata ya Murongo, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Lugenzi wakati wa mkutano wa hadhara wa Kijiji hicho.