Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu watatu wakiwa na dawa za kulevya aina ya bangi yenye uzito wa gram 600.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, SACP Ulrich Matei alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa jana majira ya saa tatu usiku wakiwa katika kijiji cha Sinjilili wilayani Chunya.

“Watuhumiwa kwa pamoja walikamatwa mnamo tarehe 27. 08 .2018 majira ya saa 21:00 usiku huko katika Kijiji cha Sinjilili, Kata ya Itewe, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya.

Aidha, Kamanda Matei amesema kuwa watuhumiwa hao wanaofahamika kwa majina ya Aman Gerald Mwampashi [30] Mkazi wa Sinjilili. Furaha Mwasegema [23] Mkazi wa Sinjilili. Philipo Elia [31] Mkazi wa Sinjilili, watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Hata hivyo, Matei ameongeza kuwa jeshi la Polisi linaendelea na operesheni mbalimbali katika maeneo ya mkoa huo ili kuzuia na kudhibiti matukio ya uhalifu pamoja na ajali za barabarani.

 

Ghana yapokwa nafasi ya kuandaa michuano ya mataifa Afrika kwa wanawake
Harry Kane atuma salamu kwa wapinzani