Jeshi la Polisi mkoani Arusha linamshikilia Mbise Sanare Lekumo (30), mkazi wa Olasiti kwa kuhusika na mauaji ya wanawake mara kwa mara, baada ya jeshi hilo kufanya uchunguzi wa kesi za mauaji ya wanawake mkoani humo.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Salum Hamduni amesema kuwa baada ya kumkamata Mbise alikiri kuhusika na mauaji mbalimbali na kutaja mtandao wake unaojihusiha na mauaji akiwemo Lembeka Olomorojo (65), mkazi wa Osunyai na mganga wa kienyeji Bashiri Msuya (64), mkazi wa mtaa wa Kirika B Kata ya Osun.
Kamanda Hamduni amesema chanzo cha mauaji hayo ni kutokana na imani za kishirikina.
Mnamo Januari 25 2021 liliripotiwa tukio la mwanamke Anna Edward (40), mkazi wa Arusha na tarehe 31 Januari wanawake walifunga barabara ili kufikisha ujumbe kwa serikali kuhusiana na kifo cha kutatanisha cha mwanamke Anna.